35% Complete (success)
20% Complete (warning)
10% Complete (danger)
Nyumbani Jisajili Ingia
Brand

Vigezo vya matumizi ya mtandao huu

1. Mtumiaji wa mtandao wetu lazima awe na umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea, hii ni kwa ajili ya kuepuka usumbufu unaoweza jitokeza, tafadhali zingatia.

2. Mtumiaji wa mtandao wetu ni lazima awe na akili timamu, hii ni kuweza epuka usumbufu na matatizo yanayoweza jitokeza katika matumizi ya mtandao huu au hapo baadaye.

3. Mtumiaji wa mtandao wetu ni lazima awe anajua kuandika na kusoma, hii ni muhimu ili kuweza rahisisha mawasiliano katika shughuli mbalimbali za mtandao huu.

4. Mtu yeyote anao uwezo wa kutumia mtandao huu, endapo amekidhi vigezo nambari 1, 2 na 3 vilivyo orodheshwa hapo juu.

Masharti ya matumizi ya mtandao huu

1. Tafadhali hakikisha taarifa zako unazo ziweka humu ni sahihi na za kweli, hii itasaidi kukuza uaminifu kati ya wauzaji na wanunuzi katika mtandao wetu, ili kuweza fikia lengo la kukuza soko letu la ndani na kuboresha shughuli na huduma za kibiashara kupitia mtandao huu.

2. Tafadhali hairuhusiwi kutumia huduma za mtandao huu kwa akaunti isiyo ya kwako (akaunti ya mtu mwingine), hii itapelekea kufungwa kabisa kwa akaunti hiyo husika.

3. Tafadhali kama mtumiaji, wewe ni mtu muhimu sana kwetu, hivyo tunawajibika kutunza taarifa zako binafsi na nyinginezo kama vile manunuzi na taarifa za shughuli mbalimbali unazo zifanya ndani ya mtandao huu. Hivyo ili kuendelea kuzilinda taarifa hizi hakikisha unaweka taarifa zako siri na usimpe mtu mwingine.

4. Tafadhali ili kukuza ushirikiano na uaminifu katika shughuli mbalimbali ndani ya mtando huu, hakikisha bishara utakayo ifanya ni halali (sio haramu) na iwe imethibitishwa na mamlaka husika.

5. Tafadhali, haturuhusu kuuza na kununua bidhaa hatarishi kama vile silaha, vifaa vilivyo chini ya kiwango, vyakula na madawa yaliyo kwisha muda wake, hii ni kwa ajili ya usalama wa watumiaji na afya zao, tunaomba usisite kutoa taarifa kwa yeyote atakaye patikana akikiuka sheria hii.

6. Wewe kama mteja tunaomba usisite kutoa taarifa kama muuzaji uliye nunua bidhaa toka kwake haku kutendea haki, tafadhali toa taarifa ili tuweze chukua hatua mapema kabla wengi hawaja athirika na tatizo kama lako.

7. Wewe kama muuzaji ndani ya mtandao huu, unawajibu wa kumtumia mteja bidhaa yake pindi tu, utakapo pokea malipo ya bidhaa hiyo. Kuchelewesha kutuma bidhaa bila sababu muhimu kutakupunguzia heshima na kupelekea kufungiwa stoo yako au faini.

8. Tafadhali, haturuhusu matumizi ya lugha za matusi ndani ya mtandao huu au kuweka picha zenye maudhui yasiyo na maadili. Mfano kutangaza mavazi ya ndani, mavazi ya kimitindo n.k kunatakiwa kufanyike kwa kuzingatia maadili.

9. Tafadhali, haturuhusu matumizi ya taarifa za mtu mwingine bila ruhusa toka kwake, kama vile picha, kazi zenye hati miliki, Michoro, Nembo n.k.

Kuhusu mabadiliko ya vigezo na masharti yetu

1. Vigezo na masharti ya matumizi ya mtandao wetu yanaweza badilishwa muda wowote ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu na pia kuendana na usalama, viwango na sheria mpya za matumizi ya kimitandao na mawasiliano pale itakapo tubidi. Ikitokea mabadiliko yamefanyika wateja wetu mta tumiwa ujumbe wa SMS kwenye simu yako na message kwenye akaunti yako, utakao wajulisha juu ya mabadiliko hayo mapya.

Usalama wako mtandaoni na wa taarifa zako

1. Ukiwa kama mteja wetu tunakuhakikishia kuwa taarifa unazoziweka katika mtandao huu, hazipelekwi wala kutumika sehemu nyingine yeyote nje ya mtandao huu. Taarifa hizi ni siri kati yako na sisi na hakutakuwa na mtu mwingine wa tatu. Tunajitahidi kuimalisha ulinzi katika mifumo yetu na hakikisha haumpi mtu yeyote tarifa zako.

2. Tafadhali kuwa makini unapo fanya manunuzi toka stoo mbalimbali hakikisha kabla ya kununua bidhaa uwe umepata taarifa kamili na sahihi juu ya hiyo bidhaa unayo taka kuinunua, pia hakikisha muuzaji wa bidhaa ni halali, hatuto husika na utapeli wowote utakao tokea baina ya wewe na muuzaji.

Shukrani sana, tunakutakia matumizi mema ya mtandao wetu


Warning: session_start(): Cannot start session when headers already sent in /home/u777489398/domains/stooyangu.com/public_html/footer.php on line 3